April 25, 2014

MARSH (KULIA) AKIWA NA BOSI WAKE ENZI HIZO, KIM POULSEN.

Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Sylvester Marsh amesema kuwa baada ya afya yake kuimarika, yupo nyumbani amepumzika, lakini amewashukuru wote waliokuwa naye alipokuwa amelazwa.


Marsh aliyeugua na kulazwa hospitali mbili zaidi ya miezi miwili jijini Dar es Salaam, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa ambao ulisababisha kushindwa kula kutokana na uvimbe kwenye koo.

 Marsh alisema yuko kwake jijini Mwanza kwa mapumziko ya muda mrefu kabla ya kurejea kazini.


“Kwa sasa naendelea vizuri, nashukuru Mungu nilitoka hospitali, nawashukuru kwa pamoja wote waliokuwa nami kipindi cha kuugua kwangu kwa kuweza kunijulia hali na kunisaidia, Mungu awabariki,” alisema Marsh.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic