April 4, 2014

ABDULFATAH (KULIA) AKIWA NA KASEJA

Meneja wa kipa nyota, Juma Kaseja amesema yuko tayari kutoa dau mara mbili kwa mtu yeyote mwenye ushahidi kuwa kipa huyo alipokea hongo kama anavyotuhumiwa.

Abdulfatah ambaye ni mdau wa soka, amesema amesikitishwa na tuhuma za Kaseja kwamba alipokea hongo kuifungisha Yanga wakati ikicheza na Mgambo katika mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo mabingwa hao walipoteza kwa mabao 2-1, wiki iliyopita.

Abdulfatah ambaye ni mdau mkubwa wa soka, amesema Kaseja anaamini kipa huyo nyota ni mwadilifu na watu wamekuwa wkaimpakazia.
“Kama kuna mtu ana uhakika kweli alitoa hongo na Kaseja akapokea, ana uhakika na hilo basi ajitokeze na mimi nitakuwa tayari kutoa mara mbili ya kiwango alichotoa.

“Nina uhakika na hili, lakini nimekuwa nikisikitishwa sana na kuhusiana na hali inavyokwenda na Kaseja anachafuliwa.
“Hakuna anayethamini mchango wake kwa taifa au vingine, watu wanasema mambo bila ya kuwa na uhakika.

“Kama ni kukosea, Kaseja alikosea kweli na kosa alilofanya anaweza kufanya kipa yeyote lakini si hujuma,” alisisitiza.
Kumekuwa na taarifa hizo za hujuma ambazo zinawalenga Kaseja na beki Kelvin Yondani.
Lakini uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa hakuna lolote kuhusiana na hujuma na badala yake ni makosa ya kimchezo.

Hata hivyo taarifa hizo za uongozi, zimekuwa hazikubaliwi na baadhi ya mashabiki na baadhi ya wanachama ambao wanapingana na hilo.

1 COMMENTS:

  1. Kosa alilofanya ni la kizembe linaloashiria mazingira ya rushwa kutokana kufanywa na kipa mzoefu ktk mazingira magumu ya kutafuta ubingwa mbona mechi ya bonanza la nani? Mtani jembe alichukuliwa poa badala ya kumtetea mkanye.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic