April 4, 2014


Uongozi wa Yanga umesema kiungo mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi anasumbuliwa na maumivu ya enka.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema pamoja na kuzagaa kwa taarifa mbalimbali, lakini Okwi ni mgonjwa.

“Mambo mengi sana yameelezwa, lakini ukweli Okwi ni mgonjwa na hakuna suala lingine.
“Unajua wanasema maneno ya kila namna, lakini alikuwa anasumbuliwa na enka. Hata wakati anakwenda Tanga alikuwa na maumivu makali sana,” alisema Njovu.
Taarifa zilizopo, zinaeleza Okwi anaidai Yanga dola 40,000 ambazo hakumaliziwa kwenye usajili wake uliogharimu zaidi ya dola 100,000 ndiyo maana amekuwa akisusia mazoezi.
Siku nzima leo, simu ya Okwi ilikuwa inaita bila ya kupolekewa lakini kuna taarifa zimeeleza kuwa amekuwa hapokei hata simu za viongozi wa Yanga.
Lakini Njovu akasisitiza wamekuwa wakiwasiliana na Okwi bila ya matatizo na wanajua kinachombua na hasa ni suala la maumivu na si vinginevyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic