April 5, 2014


Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema hata kama hawana nafasi ya kutwaa ubingwa lakini wanachotaka ni kushinda mechi ya leo dhidi ya Kagera Sugar.

Loga amesema anaamini Simba ni klabu kubwa na wanahitaji kuendelea kuilinda heshima yake bila ya kujali wako katika wakati gani.
“Hatuko katika nafasi nzuri ya ubingwa, lakini Simba inahitaji heshima na hili ni suala ala kulifanyia kazi," alisema.

Simba iko mjini Bukoba kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itapigwa leo mjini humo. Simba itawakosa wachezaji wake muhimu Amissi Tambwe na na Joseph Owino.

“Lazima tushinde ingawa mechi itakuwa ngumu kwa kuwa Kagera ni moja ya timu bora lakini vijana wangu wako vizuri.
“Najua hata Kagera wanahitaji heshima, hivyo itakuwa ni vita ya timu mbili zinazogombea heshima,” alisema Loga.
Nafasi ya ubingwa iko kwa timu tatu ambazo ni Azam FC yenye nafasi kubwa, Yanga na kidogo Mbeya City.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic