April 18, 2014


Rais wa TFF, Jamal Malinzi amekubali kuwa kuna mchezo mchafu wa baadhi ya waamuzi kuchukua rushwa.

Malinzi amesema kuna waamuzi ambao si waaminifu wanaofanya mchezo huo mchafu lakini akasisitiza, siku itafika tu.
“Kweli si kitu kizuri na kinaturudisha nyuma, lakini siku itafika tu. Nikimkamata mtu, atakuwa mfano kwa wengine, wewe ngoja tu,” alisema Malinzi wakati akifanya mahojiano na Radio One.

Baadhi ya waamuzi wamekuwa wakishutumiwa kuchukua mlungula kutoka kwa baadhi ya klabu na kuzisaidia.

Hata hivyo, baadhi ya waamuzi wamekuwa wakipinga na maofisa wengine wakidai suala hilo ni kama kuwachafua.

Lakini kitendo cha Rais wa TFF kulikubali hadharani na kutangaza vita kwa wanaohusika, huenda ikawa ni sehemu ya dawa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic