Yanga imekata rufaa kwa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) ikipinga usajili wa Mohammed NEto wa Mgambo.
Katika rufaa ya Yanga kwenda TFF
imeeleza kuwa Neto ni raia wa kigeni lakini amesajiliwa kama raia wa Tanzania.
Kutokana na hatua hiyo, Yanga imetaka kurudishiwa
pointi tatu ilizozipata Mgambo baada ya kuwafunga mabingwa hao mabao 2-1 mjini
Tanga, wiki iliyopita.
Neto alicheza kwa dakika 32 na kutolewa
kwa kadi nyekundu baada ya kuelezwa kuwa alikuwa na hirizi.
Lakini siku moja baadaye akaibuka na
kusema hakuwa na hirizi wala kitu cha ncha kali kama ilivyoelezwa, lakini
kumekuwa na wachezaji wakubwa wanaocheza na hirizi lakini hawaripotiwi.
Yanga inachuana na Azam FC kileleni
kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kama itapewa pointi hizo tatu, itakuwa imezidi
kunogesha mbio za ubingwa huo.
Azam FC inaongoza ikiwa na pointi 53
katika mechi 23 ilizocheza na Yanga ni ya pili ikiwa na pointi 46 katika mechi
22.
Mfa maji haachi kutapatapa kwani yanga hawakiliona hili mzunguko wa kwanza waliposhinda bao 3 bila mbona yanga wanataka walete uhuni na pia mchezaji aliposajiliwa c kulikuwa na mda wa kuweka pingamizi mda huo yanga walikuwepo wapi wasiweke pingamizi ? Mpira wa bongo bwana magumashi kibao, bila shaka wameshapew mchongo na baadh ya viongozi wa TFF wenye mapenz na yanga
ReplyDelete