KOCHA VAN PLUIJM ALIONYESHA KUCHUKIZWA NA KOSA NA YONDANI LILILOZAA PENALTI KATIKA MECHI HIYO YA MGAMBO, BAADA YA MECHI ALITUMIA ZAIDI YA DAKIKA TANO AKIMUELEZEA ALICHOKOSEA. |
Beki Kelvin
Yondani hajulikani alipo, uongozi haujui na hata benchi la ufundi halitaki
kulizungumzia suala lake.
Kocha
Msaidizi, Charles Boniface Mkwasa amesema hajui lolote kuhusiana na beki huyo
na asingependa kuzungumzia.
“Sina
taarifa yoyote kuhusiana na na Yondani,” alisema.
Lakini alipoulizwa
bosi wake, Hans ven der Pluijm, naye alisema anachofanya ni kufanya wachezaji
waliopo.
“Sasa
nisingependa kumzungumzia Yondani, waliopo ndiyo ninafanya nao kazi na nguvu
tunaelekeza katika mechi zilizobaki na tunataka kushinda zote,” alisema.
Viongozi wamekuwa
wakikwepa kulizungumzia, lakini Yondani inaelezwa aliondoka mara tu baada ya
mechi ya Mgambo ambayo Yanga ililala kwa mabao 2-1 mjini Tanga.
Rafiki wa
karibu wa Yondani, ameiambia SALEHJEMBE kwamba, beki huyo alikasirishwa na
kuvishwa lawama alizoona hazikuwa na msingi, kwamba alihujumu kwa kuwa
alisababisha penalty iliyozaa bao la pili.
“Unajua
yeye ni beki, kosa linaweza kutokea na anaona anaonewa bila sababu za msingi na
mbaya kuna baadhi ya viongozi wanaonekana kuungana na wale wasiojua mpira na
kusisitiza alisababisha penalty kwa makusudi.
“Sasa hali
hiyo imemuudhi na ukizingatia alicheza kwa nguvu sana, alijituma sana siku ile
kwa kuwa anajua umuhimu wa ubingwa,” alisema rafiki yake huyo wa karibu bila ya
kusema Yondani amejijimbia wapi.
Kabla ya
kujiunga na Yanga, wakati huo akiwa Simba, Yondani alikimbilia kwao Mwanza na
kujichimbia chanzo likiwa suala la lawama na kushutumiwa kuwa aliifungisha
Simba makusudi.
0 COMMENTS:
Post a Comment