Beki wa kushoto wa Yanga, David Luhende, ambaye mkataba wake na
klabu hiyo unafikia tamati mwishoni mwa mwezi huu, amedai uongozi wa timu hiyo
umempotezea.
Hali hiyo imefanya
Luhende kuwa na wasiwasi ikiwa ni pamoja na kuanza kuamini tetesi zilizopo hivi
sasa kuwa, jina lake ni moja ya majina ya wachezaji wa klabu hiyo watakaoachwa
kama ilivyopendekezwa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van Der
Pluijm, baada ya kumalizika kwa michuano ya ligi kuu hivi karibuni.
Luhende amesema mpaka sasa
hajui chochote kuhusiana na hatima yake katika kikosi cha Yanga kwani uongozi
wa klabu hiyo haujaonyesha dalili zozote za kutaka kumwongezea mkataba.
Alisema hali hiyo inamfanya awe na wasiwasi kuna uwezekano mkubwa
msimu ujao asiwe na kikosi cha timu hiyo katika michuano ya ligi kuu
inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti, mwaka huu.
“Hivi sasa nipo nyumbani ninaendelea kujifua mwenyewe kwa lengo la
kujiweka fiti, japokuwa mpaka sasa sijui chochote kuhusiana na hatima yangu
katika kikosi cha Yanga.
“Nasema hivyo kwa sababu mpaka sasa bado hawajaniita kwa lengo la
kuingia nao mkataba mpya kutokana na ule wa sasa kufikia tamati mwishoni mwa
mwezi huu,” alisema Luhende.
Hata hivyo, alipoulizwa ni kwa nini hajaitwa, alisema hajui
chochote lakini alidai kuwa anaendelea kuwasikiliza kabla ya kuchukua uamuzi
mwingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment