Pamoja na hofu hasa baada ya kuonekana akiwa kwenye
kiti cha wagonjwa cha magurudumu, Luis Suarez ameendelea kusisitiza atacheza
Kombe la Dunia.
Daktari wa timu ya taifa ya Uruguay, Alberto Pan atazungumza
leo na kueleza nini kitatokea kwa Suarez lakini tayari amefanyiwa upasuaji.
Mashabiki na waandishi wa habari walijazana katika
hospitali ya Medica Uruguaya.
Huku akisindikizwa na madaktari wengine wa timu ya
taifa, Suarez alionekana kuwa mtulivu kupita kiasi.
0 COMMENTS:
Post a Comment