Mgombea aliyeenguliwa katika kiti cha
urais wa Simba, Michael Richard Wambura, amekumbana na kizingiti kingine katika
uchaguzi mkuu wa klabu hiyo, jana Jumapili.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye
Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar, Wambura alizuiwa getini
wakati akiwa kwenye foleni akijiandaa kuingia ndani ya ukumbi.
Mara
baada ya kuzuiwa, Wambura alisema amezuiwa kutokana na jina lake kutotokea
katika orodha ya wanachama wa klabu hiyo, hivyo anashangaa kitendo hicho
kilichotokea ambacho siyo sahihi huku akidai kuwa yeye ni mwanachama halali wa
Simba.
“Kiukweli nasikitika sana kwa kitendo hiki
kilichotokea cha kuzuiwa mlangoni wakati najiandaa kuingia kwenye ukumbi wa
kupigia kura, eti wanasema jina langu halionekani katika mtandao.
“Mimi sina jinsi, nimeona ni bora
niondoke zangu, lakini ninaendelea kuchunguza kujua kilichotokea, mimi ninajua
ni mwanachama halali wa Simba,” alisema Wambura akionyesha kusikitishwa na jambo hilo.
Awali Wambura alienguliwa kushiriki uchaguzi huo baada ya kujitokeza akiwania nafasi ya urais na mwisho wanachama wakatinga mahakamani lakini pia wakashindwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment