Kampeni ya shindano
la kwenda nchini Brazil kushuhudia fainali ya Kombe la Dunia inayojulikana kwa
jina la Brazuka imepata washindi nane wa awali ambao jana walikabidhiwa zawadi
zao.
Zawadi
walizopewa washindi hao kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Esacape
One, Kawe jijini Dar ilikuwa ni pamoja na jezi mpya za timu za taifa
zitakazotumika kwenye michuano hiyo, fedha taslimu shilingi 50,000 na simu.
MULLY AKIKABIDHI JEZI |
Washindi
hao waliohudhuria na kukabidhiwa zawadi hizo walikuwa Rose Kyaso, Isihaka
Masheu, Emmnauel Mkengere na Eric Vemberini na walioshindwa kuhudhuria kutokana
na udhuru maalum walioutoa ni pamoja na Ramson Waruto, Alfred Ngonya, Hawa Said
na Pius Joseph.
Mratibu wa
kampeni hiyo ya Brazuka, Lumuliko Mengele ‘Mully B’ alisema washindi ambao
hawakufika watatumiwa zawadi zao huko walipo kwani wengi wanaishi mikoani.
“Hawa ni
washindi wetu wa awali lakini kutakuwa na wengine watakaopatikana kwenye droo
itakayochezeshwa Ijumaa ya tarehe sita ambao watakwenda kushuhudia mechi ya tarehe
16 na pia Jumatatu ya tarehe tisa kutakuwa na droo nyingine pia ya washindi
watakaokwenda kushuhudia mechi ya tarehe 21.
“Lakini
baadae kutakuwa na droo ya kuwatafuta washindi watakaoshuhudia robo fainali na
nusu fainali, tunawataka watu waendelee kushiriki kwa kuwa bado kuna zawadi
nyingi na safari kama hizi za Brazil tutawagharamia kila kitu mpaka siku
watakayorejea nchini. Unaweza kushiriki kwa kutuma neno Brazuka kwenda namba
15678,” alisema Mully B
0 COMMENTS:
Post a Comment