Kocha Mkuu
wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema kazi dhidi ya Msumbiji haitakuwa lelemama na
kunatakiwa kuwa na maandalizi ya kutosha.
Stars
inakutana na Msumbiji katika kuwania kucheza kwenye makundi ya Kombe la Mataifa
Afrika litakalofanyika mwakani nchini Morocco.
Nooij
aliyewahi kuwa kocha wa Msumbiji amesema wamakonde hao wanaichukulia mechi hiyo
kwa uzito wa juu.
“Haitakuwa
mechi lahisi kama wengi wanavyodhani, lakini tuna kikosi bora ambacho
kinahitaji maandalizi bora.
“Itakuwa ni
vita ya kimichezo na lazima tujiandae ili tushinde kwa kuwa Watanzania
wanaotuunga mkono wanatak kwenda mbali,” alisema Nooij raia wa Uholanzi.
Stars
imefanikiwa kuing’oa Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2 na sasa inakumbana na
Msumbiji katika mechi mbili nyumbani na ugenini kuwania kucheza hatua ya
makundi Afcon.
0 COMMENTS:
Post a Comment