Mshambuliaji
nyota wa Chelsea, Andre Schurrle amesema amekuwa akiendelea kufuliwa nguo zake
na mama mzazi.
Pamoja na kuwa ‘jibaba’
anayelipwa pauni 73,000 kwa wiki katika kikosi cha Chelsea, Schurrle amesema
mama yake ndiye amekuwa akimtegemea kwa usafi.
“Ninajisikia na
amani sana ninapokuwa karibu na wazazi wangu.
“Nikiwa London
ndiyo naweza kufanya usafi, tofauti na hapa nyumbani (Ujerumani), kila kitu
hadi kufua nguo anafanya mama,” anasema mshambuliaji huyo mwenye miaka 23.
“Napenda kukaa
na wazazi wangu, maisha yanakuwa na amani zaidi,” anasema Schurrle ambaye hivi
karibuni aligoma kununua nyumba jijini London.
0 COMMENTS:
Post a Comment