Kiungo mwenye
kasi na vyenga vya maudhi, Arjen Robben nusura azichape na mwenzake wa kikosi
cha Uholanzi kwa madai anamchezea undava.
Wawili hao wako katika kikosi cha Uholanzi ambacho imetua nchini Brazil mapema kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya Kombe la Dunia na wako kundi moja na mabingwa watetezi, Hispania ambao walicheza nao fainali mwaka 2010 na kupoteza kwa bao 1-0.
Robben
anayekipiga Bayern Munich alilasirishwa na beki Bruno Martins Indi kwamba
anamchezea kindava hadi akataka wazichape.
Lakini Indi
naye alimlaumu kiungo huyo kwa kujiangusha bila ya sababu za msingi wakati
akijua wako mazoezini.
Mara ya kwanza,
Robben alitibiwa kidogo na kuendelea na baadaye akatibiwa byumbani kabla ya
kurudi uwanjani.
Beki huyo wa Feyenoord
ya Uholanzi alionyesha pia kuchukizwa na Robben kutumia staili yake ya
kujiangusha kila akigushwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment