Nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo
ameonekana akiwa na mpenzi wake Irina Shayk ambaye ni mwanamitindo maarufu walipokwenda kushuhudia pambano
kali la ngumi za kulipwa kati ya Miguel Cotto dhidi ya Sergio Martinez.
Ronaldo ambaye
yuko katika maandalizi ya mwisho ya Kombe la Dunia, alitua kwenye ukumbi
maarufu duniani wa Madison Square Garden jijini New York, Marekani akiwa na
mpenzi wake huyo na kushuhudia pambano kali, ambapo Cotto alimchakaza Martinez
na kubeba ubingwa wa dunia wa WBC katika uzito wa middle.
Ronaldo, 29,
alikuwa katika ya nyota kivutio waliokuwa kwenye pambano hilo, huku mwingine
akiwa ni maarufu 50 Cent.
0 COMMENTS:
Post a Comment