June 10, 2014



Michael Wambura amerudishwa kugombea urais Simba kupitia kura.
Kamati ya rufaa ya TFF, kupitia mwenyekiti wake, Julius Lugaziya imemrudisha Wambura na kesho saa 5 asubuhi itatangazwa.
Blogu hii ilieleza leo mchana kuhusiana na suala la Wambura kuwa gumu na kufikia kwenye uamuzi wa kura.
Hata hivyo, suala hilo limeonyesha kuwachanganya wengi kama kweli kura inaweza kutumika katika suala la kisheria.
Lakini sasa Wambura atapambana na Avens Aveva kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais wa klabu maarufu ya Simba.
Awali, Wambura aling’olewa kuwania urais baada ya kubainika uanachama wake una walakini.
Kamati ya uchaguzi ya Simba chini ya mwanasheria maarufu, Dokta Damas Daniel Ndumbaro ilibaini kuwa uanachama wake una walakini na mkutano mkuu wa Simba pekee ndiyo wenye uwezo wa kurekebisha jambo hilo.

2 COMMENTS:

  1. kwa mantiki hii mpira wa Bongo haufuati sheria ila brabra!

    ReplyDelete
  2. mambo ya kisheria kuamuliwa kwa kura! Haya ni maajabu ya dunia na yanatokea TZ tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic