June 3, 2014




Kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema amebakiza siku chache kabla ya kuondoka kwenda Saudi Arabia kuanza kazi mpya.


Pluijm ambaye amepata kazi nchini humo, amesema ataanza kazi hiyo siku chache zijazo baada ya kumalizana na familia yake.
Pluijm raia wa Uholanzi amekuwa akiishi nchini Ghana kwa zaidi ya miaka nane sasa.

“Siku zinahesabika hapa Ghana, safari ya Saudi Arabia itaanza kwa ajili ya kazi mpya,” alisema kutoka Accra.
“Ilikuwa ni lazima nianze mapema kwa kuwa kazi ni mpya na ninahitaji kujifunza zaidi na mambo ni mengi,” aliongeza.
Kocha huyo aliamua kuchukua mkataba mpya baada ya Yanga kuzubaa katika  suala la kumuongezea mkataba, lakini taarifa nyingine zinaeleza, dau la Waarabu lilikuwa kubwa zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic