Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limepokea taarifa za kutolewa
wito bungeni wa
kulitaka litumie tiketi za elektroniki katika kukusanya
mapato.
Tunataka
ieleweke wazi kwa umma wa Watanzania kuwa si nia yetu
kuchelewesha matumizi ya
uingiaji mpirani kwa tiketi za elektroniki. Ieleweke
kuwa mfumo wa kuingia
kwenye mbuga, KCMC, mipakani ni tofauti na uingiaji
mpirani.
Katika
mpira wa miguu wanaingia maelfu ya watu katika kipindi kifupi. Kwa kuzingatia
umuhimu wa kulinda usalama wa watazamaji na miundombinu ya viwanja ndio maana
tulisitisha matumizi ya tiketi za elektroniki hadi tujihakikishie usalama wa
matumizi yake.
Tunafanya
jitihada kwa karibu na mzabuni benki ya CRDB ili kuhakikisha mfumo huu unaanza
kutumika mara moja.
Kwa niaba ya sekta ya
michezo tunatoa wito kwa Serikali kushusha au kuondoa kodi kubwa zinazotozwa
kwenye vifaa vya michezo, hasa vinavyotumiwa na watoto kuanzia umri wa miaka
6-12, ili watoto wetu waweze kuvipata kirahisi toka kwa wazazi wao ili waweze
kujifunza kucheza michezo kisasa tangu wakiwa wadogo.
0 COMMENTS:
Post a Comment