June 2, 2014


Timu ya taifa ya vijana wa chini ya miaka 15 imewasili jioni hii ikitokea nchini Botswana ambapo ilikuwa ikishiriki michuano ya vijana.
Timu hiyo ilifanikiwa kufika fainali lakini ikaambulia nafasi ya pili baada ya kupigwa na Nigeria kwa mabao 2-0. 
Timu zilizoshiriki michuano hiyo zililalamika kuwa Nigeria walipeleka vijeba.
Baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, vijana hao walipokewa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na ndugu zao ambao waliwafika mashada ya maua.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic