MAXIMO...CHOZI |
Unaweza kuona maajabu, lakini ndiyo
imetokea kwa kocha wa klabu kujikuta akidondosha chozi baada ya kuona timu ya
taifa ikitoka sare.
WAMEONA WAMUACHE KIDOGO APUMZIKE... |
Stori hiyo ya Maximo kuangua kilio imeripotiwa na gazeti la Championi Jumatatu.
Katika pambano hilo lililomalizika
kwa sare ya mabao 2-2, Maximo aliyekuwa amekaa eneo la VIP akiwa ameongozana na
wakala wake aitwaye Ally na msaidizi wake, Leonaldo Leiva, alishindwa kuinuka
akibaki kwenye kiti chake kwa takribani dakika 15.
Wakati mashabiki wameishaondoka
uwanjani hapo, Maximo aliendelea kubaki uwanjani akiwa amekaa kwenye kiti na
Leiva na Ally walilazimika kumbembeleza na kumuomba waondoke, lakini yeye
akamwaga chozi.
BADO HAKIJAELEWEKA.. |
Muda mwingi Maximo alikuwa akilalama
akionyesha kukerwa na Msumbiji kusawazisha bao katika dakika ya 87 na kuufanya
mchezo wa marudiano jijini Maputo kuwa mgumu.
Maximo aliwahi kuinoa Taifa Stars
kuanzia mwaka 2006 hadi 2010, hali iliyoonyesha alikerwa na sare hiyo na hasa
bao la kusawazisha.
MWISHO KAKUBALI WANAONDOKA... |
Baada ya wenzake kumbembeleza na
kumshindwa, waliamua kumuacha kwa muda huku uwanjani hapo watu wakiwa wameishaondoka.
Muda mchache wa takribani dakika sita
au saba waliomuacha atafakari, walirudi tena na kumsihi waondoke uwanjani hapo,
ndipo akakubali.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza Maximo
kukiona kikosi cha Taifa Stars kikicheza tena baada ya miaka minne, tokea
alipoondoka.
Maximo ambaye anaendelea kuinoa Yanga
kujiandaa na msimu mpya, huenda ni mapenzi yake kwa Stars ndiyo yaliyofanya
amwage chozi au mapenzi yake tu na soka la Tanzania au kumbukumbu ya kipigo cha
bao 1-0 dhidi ya Msumbiji alichokipata wakati wa ufunguzi wa Uwanja wa Taifa,
mfungaji akiwa Manuel Jose Bucuane ‘Tico-tico’.
0 COMMENTS:
Post a Comment