Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema
huu si wakati wa wachezaji wengi kufanya majaribio katika kikosi chake.
Logarusic amesema atawapunguza wachezaji karibu
wote waliokwenda kufanya majaribio katika kikosi chake.
“Kama kuna mchezaji tunamhitaji kwenye nafasi
fulani, tayari ninajua kuhusiana na uwezo wake hapo itakuwa sahihi kwa kuwa
nitataka kujiridhisha.
“Lakini suala la kutaka kuwaona wachezaji
wanafanya nini au ndiyo watumie muda mwingi wa majaribio, sasa si wakati wake.
“Kipindi hiki ni kwa ajili ya maandalizi ya
msimu na tunatakiwa kuwa makini kwa kuwa ukicheza sasa, ujue umepotea msimu
mzima,” alisema Logarusic.
Simba inafanya mazoezi yake kwenye gym ya Chang’ombe
na jioni imekuwa ikijifua kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
0 COMMENTS:
Post a Comment