BRAZIL |
WAKATI wa mechi za Ligi Kuu Bara,
wafanyabiashara hutegemea kuuza ice cream, machungwa, jezi na vitu vingine
vidogovidogo.
Wakati wa Kombe la Dunia, mambo huwa
tofauti na safari hii nchini Brazil, vitu ambavyo vimekamata mauzo vimekuwa si
vile vilivyotarajiwa.
ARGENTINA |
Jezi za mbwa:
Kawaida ubunifu ni kitu bora, watu wengi
wa Ulaya na Amerika Kusini huongozana na wanyama na hasa mbwa.
Wengi huwanunulia jezi ili kuendena na
muonekano wa mashindano kama hayo ya Kombe la Dunia.
ITALIA |
Jezi ya Neymar yenye namba 10 ndiyo
imeshika namba moja kutokana na mashabiki wengi kuwanunulia mbwa wao.
Mbwa wadogo na wale wakubwa wameonekana
kwa wingi wakiwa wamevaa jezi hizo za Neymar zenye namba 10 mgongoni.
Kila jezi imekuwa ikiuzwa kwa fedha
inayolingana na dola 1o tu (Sh 16,5000). Na wengi wameonekana kuvutiwa na jezi
ya Neymar.
HISPANIA&UHOLANZI |
Kondom:
Kila yanapofanyika mashindano makubwa,
kumekuwa na utaratibu wa kutengeneza mipira ya kiume maalum kwa ajili ya
michuano hiyo.
Ilitengenezwa mipira 850,000 ya kiume
kwa ajili ya michuano hiyo. Kila pakti moja yenye mipira mitatu imekuwa ikiuzwa
kwa dola 1.39 katika maduka mbalimbali hasa katika miji ambayo mechi za Kombe
la Dunia, zinapigwa.
Mipira hiyo ya kiume maarufu kama
kondomu imekuwa kati ya vitu vilivyonunuliwa kwa wingi zaidi kwa kuwa yote
850,000 imeisha hata kabla ya kuanza kwa hatua ya robo fainali hiyo jana.
ENGLAND |
Bosi wa kampuni ya DKT International,
Daniel Marun amesema: “Imekwisha na tunalazimika kuagiza idadi kama hiyo
iliyoisha, huenda watu wengi wananunua kwa wingi kwa ajili ya kupeleka zawadi
watakaporejea nyumbani.”
Pamoja
na mauzo hayo ya juu ya kondomu katika Kombe la Dunia, inaelezwa rekodi hiyo
itavunjwa wakati wa Michezo ya Olimpiki ya kipindi cha joto itakayofanyika
mwaka 2016.
UJERUMANI |
Stika za
Panini:
Zimekuwa zikitengenezwa tokea Kombe la
Dunia mwaka 1970. Hizi ni zile picha za wachezaji ambazo unaweza kubandika
kwenye gari, jokofu na kwingine.
Lakini pia ziko zinazohifadhiwa kwenye
albamu na zinakuwa na picha za wachezaji wa timu mbalimbali.
Kutokana na kuuzwa sana ilifikia bei
zake zikapanda hadi dola 200 (zaidi ya Sh 340,000) kwa albamu nzima ya picha
hizo na inaelezwa mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter, ndiyo ilichangia
mauzo yake.
Jezi za
Ujerumani:
Kampuni ya
vifaa vya michezo ya Adidas, imetangaza kuwa jezi zote za
timu ya taifa ya Ujerumani zilipolekwa Brazil, zimeuzwa kwa asilimia kuanzia 80
hadi 90.
Adidas wamesema hadi itakapofikia
mabingwa kupatikana Juni 13, wanaamini watakuwa wameuza jezi milioni nane za
Ujerumani.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Adidas,
Herbert Hainer amesea wanaweza kuuza jezi milioni mbili zaidi ya hizo kama
Ujerumani itashinda mechi zake za robo na nusu fainali.
Bendera:
Bendera kubwa nyepesi ambazo zinaonekana
kwenye viwanja mbalimbali, nazo zimenunuliwa kwa kiasi kikubwa.
Mfano, baada ya Algeria kuvuka na
kuingia hatua ya 16 bora, mashabiki wa timu hiyo walikuwa wakihaha huku na kule
kuzitafuta bendera hizo tena walikuwa tayari kuzinunua mara mbili au tatu
kutoka bei ya kawaida.
Lakini bendera za nchi mbili, Hispania
na England ambazo zilikuwa zinaongoza kwa mauzo zilidorora baada ya timu zao
kutolewa mapema.
Jezi:
Kwa
upande wa jezi za wachezaji, walioshika nafasi tatu za juu ni Neymar ambaye
yuko nyumbani Brazil, Robin van Persie hasa baada ya kufunga bao la kupaa
katika mechi dhidi ya Hispania.
Lakini nahodha wa Marekani, Clint
Dempsey amewashangaza wengi baada ya kushika nafasi ya tatu kutokana na jezi
zake kununuliwa kwa wingi zaidi akienda sawa na mshambuliaji wa Mexico, Javier
Harnandez ‘Chicharito.
Kwa upande wa timu, kabla haijaondolewa
mashindano, jezi za Mexico ndiyo zilikuwa zikinunuliwa zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment