Kocha Mkuu
wa Simba, Zdravko Logarusic amesema atasikia faraja kuifunga Yanga ikiwa chini
ya kocha wao mpya, Marcio Maximo ili kulipa kisasi cha Brazil kuidhulumu
Croatia katika Kombe la Dunia.
MAXIMO |
Logarusic
maarufu kama Loga, amesema anaamini siku watakapocheza na Yanga, Maximo
hatasamilika, labda Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), liamue kuleta mwamuzi
Mjapani ambaye atakuwa tayari kuibeba Yanga kwa kuwa inafundishwa na Mbrazil.
“Nimesikia
sana kuhusiana na Maximo,” alisema Loga kutoa kwao Croatia. “Lakini sitaki
kuingilia kinachohusiana na Yanga kwa kuwa wanafanya yao na sisi Simba
tutafanya yetu.
“Ila ikifika
siku tunakutana na Yanga, nitafanya kila linalowezekana tushinde, itakuwa
furaha kwangu kwa mambo mawili. Kwanza nimefanya kazi yangu vizuri, pili
nimemshinda kocha kutoka Brazil ambaye timu yake iliidhulumu Croatia kwa kuwa
ni nwenyeji wa Kombe la Dunia.”
Loga amesema
amekuwa akifuatilia kila kitu kinachoendelea katika soka nchini licha ya kuwa
yuko kwao Croatia.
“Kila kitu
najua, nafuatilia kwa ukaribu sana kupitia mitandao. Kuhusiana na suala la
kurudi Tanzania, nafikiri itakuwa Jumatatu, bado nilikuwa nasubiri wanitumie
tiketi.
“Baada ya
kufika nitahitaji muda wa saa 24 kupumzika kabla ya kuanza kazi, kama nitafika
Jumatatu, basi mazoezi nitaanza Jumatano,” alisema Logarusic.
Kocha huyo
wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya, amesema ana imani kubwa chini ya uongozi mpya
wa Evans Aveva, Simba ina nafasi ya kufanya vziuri zaidi na kubeba ubingwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment