Pamoja na kufurahia kuingia
nusu fainali ya Kombe la Dunia ambayo waliikosa tokea mwaka 1998, mashabiki wa
Argentina wametembea na sanamu la uti wa mgongo.
Mashabiki hao wametembea na
sanamu hilo wakionyesha kufurahia kuumia kwa mshambuliaji Neymar wa Brazil.
Neymar ambaye atakosa mechi
mbili zilizobaki za Kombe la Dunia, aliumizwa na beki wa Colombia baada ya
kumngonga na goti kwenye uti wa mgongo.
Hali hiyo imesababisha
kutolewa kwa kuwa mfupa mdogo wa uti wa mgongo umevunjika.
Mashabiki hao walikuwa
wakiimba sehemu mbalimbali mitaani kueleza kuwa Brazil wamekwisha kwa kuwa
tegemo lao ameondolewa na uti wa mgongo.
0 COMMENTS:
Post a Comment