Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza Mbrazil,Genilson
Santana Santos ‘Jaja’, atasaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga.
Imeelezwa kwa kuwa Jaja ni pendeezo la Kocha Mkuu wa Yanga, hakutakuwa na haja ya kumfanyia majaribio, badala yake ni kusaini na kuanza kujifua.
Taarifa iliyoandikwa na gazeti maarufu la michezo nchini la Championi kuhusiana na Jaja, ilieleza hivi:
Jaja
ambaye anasifika kwa mashuti, pasi zinazozaa mabao, lakini amefunga zaidi ya
mabao kumi akiwa nje ya 18, maana yake akiwa fiti, akazoea mazingira, wapinzani
wakubwa wa Yanga, yaani Simba na Azam FC, watakuwa katika wakati mgumu.
Hali
inaonyesha kuwa Jaja atachukua nafasi ya Emmanuel Okwi ambaye ameonekana
kuukoroga uongozi wa Yanga mwishoni mwa msimu uliopita kutokana na kutoroka
kambini na kususa mechi za mwisho za ligi.
Katibu
Mkuu wa Yanga, amethibitisha ujio wa Jaja lakini akakataa kulizungumzia suala
la nafasi ya Okwi.
“Kweli
huyo mchezaji anayeitwa Jaja anakuja, nafikiri litakuwa ni suala la kocha kama
ataridhika naye baada ya majaribio, basi usajili utafuatia.
“Siwezi
kusema ni Jumanne au Jumatano, lakini ndani ya siku hizo mbili tunaamini atakuwa
ametua nchini,” alisema Njovu na kuongeza.
“Kuhusiana
na kuchukua nafasi ya Okwi au mchezaji mwingine, hilo tuliache kwa wanaohusika
na usajili, ukifika wakati wataluzungumzia.”
Pamoja
na Njovu kutotaka kulizungumzia hilo, lakini taarifa zinasisitiza Okwi ndiye
aliyekalia kuti kavu zaidi kutokana na kuwasumbua Yanga, kitu ambacho kinaweza
kusababisha mkataba wake kuvunjwa.
Yanga
haina ujanja, lazima italazimika kutema baadhi ya wachezaji wake wa kigeni ili
kutoa nafasi kwa wageni Wabrazil wawili, Coutinho na Jaja na inaonekana Haruna
Niyonzima na Mbuyu Twite (Rwanda) na Hamis Kiiza (Uganda) ndiyo wenye nafasi ya
kuunda nafasi tano ya wachezaji wa kimataifa wakiwa na Wabrazil hao.
Jaja
ataunga na Wabrazil wengine watatu ambao ni Kocha Marcio Maximo, msaidizi wake
Leonaldo Neiva na kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye ameanza mazoezi na
Yanga tayari.
Uongozi
wa Yanga umeamua kuimarisha benchi lake la ufundi, pia kuongeza wachezaji wa
kimataifa ili kuhakikisha inafanya vizuri msimu ujao ikiwa ni pamoja na
michuano ya kimataifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment