MWOMBEKI (KUSHOTO) AKIPAMBANA NA MABEKI WA PRISONS. |
Mshambuliaji mpya wa JKT Ruvu, Betram Mwombeki amesema yuko
katika kiwango kizuri na anatamani kukutana na Simba ya Zdravko Logarusic na
kuonyesha uwezo.
Mwombeki aliondoka Simba baada ya Loga kusisitiza
kutomtaka katika kikosi chake.
Mshambuliaji huyo alionekana msaada mkubwa kabla ya kutua
kwa Loga ambaye hakuelewana naye.
Mwombeki amesema ana mapenzi makubwa na Simba na anatamani
kurudi na kufanya kazi katika kikosi hicho.
“Uwezo ninao, ninachotaka ni kufanya vema na siku ikifika,
nitarudi tena.
“Nimefanya mazoezi sana, ninaendelea kujifua lakini lengo
ni kufanya vizuri,” alisema straika huyo ambaye alionyesha uwezo mkubwa akiwa
Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment