July 8, 2014



Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amegoma kujibu swali kuhusiana na uamuzi wa kumrejesha Mrisho Ngassa kwenye kikosi chake na kusisitiza anapaswa kujibu mwenyewe.
Nooij raia wa Uholanzi aliwaambia waandishi wa habari kwamba swali hilo kwa kuwa anajua kilichotokea.
“Siwezi kujibu, yuko hotelini. Mnaweza kumtafuta na kumuuliza kwa nini ilikuwa hivyo,” alisema Nooij.

Taifa Stars tayari ipo kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Msumbuji kuwania kufuzu kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika.

Awali Yanga ilihoji kuhusiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumruhusu Ngassa kwenda kufanya majaribio Afrika Kusini bila ya ruhusa ya klabu ambayo ilikuwa inajua yuko kambini Botswana.

Lakini Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine akasema Ngassa hakuripoti kambini tokea siku ya kwanza, hivyo TFF haijui lolote na Nooij aliamua kumuondoa na angeikosa mechi ya Msumbuji.

Lakini sasa kila mmoja amekuwa akiruka kuhusiana na suala na tayari Ngassa ameanza kujifua na Stars tayari kuivaa Msumbuji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic