Na Boniface Wambura
Wakati Taifa Stars
inaingia kambini Tukuyu mkoani Mbeya kesho (Julai 9 mwaka huu), kocha Mart
Nooij amesema kambi ya wiki mbili nchini Botswana imekisaidia kikosi chake
kujiandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam leo (Julai 8 mwaka huu) kuhusu maandalizi ya timu hiyo, Nooij
amesema timu yake inafanya mazoezi kwenye maeneo ya baridi kwa sababu za
kitaalamu, hivyo kambi ya Tukuyu kama ilivyokuwa ya Botswana itawasaidia kwa
mechi dhidi ya Msumbiji.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka kwa ndege kwenda Mbeya
ikiwa na kikosi cha wachezaji 25, na itarejea jijini Dar es Salaam siku tatu
kabla ya mechi hiyo.
Wachezaji walioko
kwenye msafara huo ni Aggrey Morris, Aishi Manula, Amri Kiemba, Benedictor
Tinoko, Deogratius Munishi, Edward Charles, Emmanuel Namwando, Erasto Nyoni,
Haruni Chanongo, Himid Mao, John Bocco na Jonas Mkude.
Wengine ni Joram
Mgeveke, Kelvin Friday, Kelvin Yondani, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Mwagane
Yeya, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Ramadhan Singano, Said Juma,
Said Moradi, Shabani Nditi, Shomari Kapombe, Simon Msuva,
Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya
kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbiji
itafanyika Julai 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment