July 31, 2014

NSAJIGWA WAKATI AKIINOA LIPULI YA IRINGA KABLA YA KUAMUA KUACHANA NAYO NA KWENDA KUCHEZA SOKA NCHINI NEPAL. SASA AMEANZA KAZI RASMI YANGA AKIWA KOCHA MSAIDIZI WA VIJANA.


Nahodha wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa, leo ameanza kazi rasmi kuinoa timu ya vijana.
Nsajigwa anakuwa kocha msaidizi wa vijana na atakuwa chini ya Leonaldo Leiva na leo beki huyo wa zamani wa kulia wa Yanga ameanza kazi.
Nsajigwa ameanza kazi wakati Yanga ilipokuwa inajifua kwenye viwanja vya Tangayika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.
Kocha wa sasa wa Yanga, Marcio Maximo alifanya kazi na Nsajigwa kwa ushirikiano wa karibu wakati wakiwa timu ya taifa, Taifa  Stars kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic