July 8, 2014

KIONGERA (KUSHOTO) AKIWA KAZINI


Mshambuliaji mpya wa Simba, Modo Kiongera anatarajia kuwasili nchini kesho au keshokutwa ili kumalizana na uongozi wa klabu hiyo.
Kiongera aliyekuwa anakipiga KCB ya Kenya, tayari mambo yako vizuri na uongozi wa Simba.
“Kiongera anatarajia kutua nchini kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na Simba.
“Mazungumzo yamekwenda vizuri limebaki suala hilo la mkataba tu,” kilieleza chanzo ndani ya Simba.
Kamati ya usajili ya Simba imekuwa ikiendeleza harakati zake za usajili kwa ajili ya kuboresha kikosi kipya.
Kiongera aliyewahi kufanya kazi na Kocha Zdrakvo Logarusic anasifika kwa mashuti makali na mipira ya vichwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic