July 8, 2014

LOGA AKIWA KWAO CROATIA

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema yuko tayari kwa kazi na atatua nchini wakati wowote ndani ya wiki hii.
Logarusic raia wa Croatia amesema amemaliza kila kitu alichotaka kufanya kwa ajili ya mapumziko na sasa amebadili mwelekeo na kuelekea kazini.

“Wakati wowote nitakuwa Tanzania, mapumziko yameisha na akili yangu imehamia kwenye kazi.

“Kila kitu ninachowaza kwa sasa ni Simba tu, najielewa kuwa mapumziko yamkwisha,” alisema.
Loga alikuwa kwao Croatia kwa mapumziko na pia alifanya ziara nchini Bosnia-Herzegovina kwa ajili ya kujipumzisha.

Simba inatarajia kuanza mazoezi wiki hii, imeelezwa baada ya hapo itakwenda kuweka kambi mjini Zanzibar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic