July 31, 2014



Wakati lisiti ya wachezaji wengine wa Real Madrid watakaokuja inasubiriwa kutajwa, sasa uhakika Luis Figo atakuwepo.

Kikosi cha wakongwe cha Real Madrid kinatarajia kucheza mechi ya kirafiki Agosti 23 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo itakuwa dhidi ya nyota wa Tanzania wakiwemo wale wanaocheza kikosi cha Taifa Stars, sasa.
Figo ni mmoja wa wachezaji wanaosubiriwa kwa hamu na mashabiki nchini.
Mratibu wa ziara hiyo, Ssebo amesema Figo ni kati ya wachezaji watakaokuwa na kikosi hicho jijini Dar.
“Kikosi chao ni kipana sana, kuna kina Owen, MacManamann, Zidane, Robertp Carlos na wengine wengi.
“Ila kuwapata wote inategemeana na majukumu fulani. Kama hawana majukumu yoyote, basi unaweza kuwapata wote.
“Sasa uhakika wa kumpata Figo upo kwa kuwa hatakuwa na majukumu wakati huo.
“Wengine pia watakuwa nyota wengi na tutaendelea kuwatangaza,” alisema Ssebo.
Mechi hiyo tayari imekuwa gumzo na Ssebo amewahakikishia mashabiki wa soka nchini kuwa kweli nyota hao watakuja nchini na wala si mzaha, hivyo wakae mkao wa kula.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic