Wabrazil
ni kati ya watu wanaoamini suala la bahati, kama ambavyo Waafrika wengi
wamekuwa wakiamini.
Wachezaji
wawili wa Yanga, Andrey Coutinho na Geilson Santana waliwasili nchini kwa nyakati
tofauti lakini kivutio wote walikuwa wamevaa mashati ya pinki.
Coutinho
alitangulia kuwasili nchini, alikuwa amevaa shati la rangi ya pinki, huenda
Yanga wangependa awe amevaa njano lakini haikuwa hivyo.
COUTINHO AKIWA NA KIZUGUTO |
Halafu
baada ya takribani wiki tatu, Jaja naye alitua nchini, akiwa na shati la rangi
ya pinki, tena iliyokolea zaidi.
Hali
hiyo ilisababisha baadhi ya mashabiki wa Yanga kuanza kuhoji vipi avae nguo
ambayo inaonekana ni kama nyekundu.
Lakini
walitulizwa na kuelezwa rangi hiyo ni pinki halafu halikuwa jambo kubwa sana.
Ukiangalia
picha za Wabrazil hao wawili utaona, kwamba hawafahamiani, lakini wote walivaa
nguo za pinki. Je, zina maana kwao hasa katika suala la bahati?
0 COMMENTS:
Post a Comment