August 7, 2014




Binti mmoja mwanafunzi wa Loyola Sekondari (jina halikufahamika), ameshindwa kujizuia na kuachana na ‘Utanzania’ baada ya kumfuata mshambuliaji wa Yanga, Coutinho na kumuambia aweze saini yake kwenye mkono wa binti.

Mara tu baada ya Yanga kumaliza mazoezi jana, binti huyo aliimfuata Coutinho na kumueleza shida yake.
Naye kwa kuwa mkononi alikuwa na viatu na chupa ya maji, haraka aliweka chini na kuweka saini yake kwenye mkono wa binti huyo.

Baada ya hapo, waliagana na kila mmoja alichukua time yake akiwa na tabasamu tele, kuonyesha wote walifurahia kilichotokea.
Watanzania wamekuwa wagumu sana kuomba saini za nyota mbalimbali kama ambavyo wamekuwa wakifanya Ulaya. Lakini binti huyo, akaachana na ‘hizo’.
Yanga imekuwa ikiendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Sekondari ya Loyola iliyoko Mabibo jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic