August 20, 2014


MWAKIBINGA (KUSHOTO) AKIWA NA MKURUGENZI WA AZAM TV, TORRINGTON, SIKU WALIPOINGIA MKATABA WA KUONYESHA LIVE LIGI KUU BARA.


Licha ya uongozi wa Yanga kuendelea kushikilia msimamo wake kukataa milioni 100 za udhamini kutoka Azam TV, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kuwa hiyo haitawazuia kuonyesha mechi zao za msimu mpya.
TFF kupitia kwa Bodi ya Ligi, ambacho ndicho chombo chenye mamlaka na Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi Daraja la Kwanza, wamesema bado milioni 100 za Yanga kutoka kwa wadhamini Azam TV, zimetunzwa wakisubiri waje kuchukua chao.
Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, amesema pamoja na Yanga kususia kitita hicho, ni lazima mechi zao ziwe live kwa mujibu wa mkataba na mdhamini.
“Fedha zao zipo benki zimetunzwa, kama unavyojua tayari AzamTV wametoa mgawo wa awali, wao hawajachukua kama walivyosusia msimu uliopita.

“Lakini hiyo haimkatazi mdhamini kuonyesha mechi zao msimu huu na nikuhakikishie lazima mechi zote zirushwe ‘live,” alisema bosi huyo.
Msimu uliopita, Yanga walikataa kuchukua milioni 100 kwa kile walichodai kuwa ni kiasi kidogo na kwamba hawawezi kuchukua kiasi sawa na timu ndogo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic