August 18, 2014



Mohammed Salim, Pemba
Kikosi cha Yanga kimewasili mjini Pemba kwa ajili ya kambi maalum kwa maandalizi ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.


Yanga wametua visiwani hapa, lakini si kikosi kizima.
Wametua kwa mafungu kwa madai ni kutokana na suala la usafiri wa ndege.

Mmoja wa viongozi amesema kuwa fungu jingine la wachezaji litawasili baadaye leo.

Yanga itakuwa hapa Pemba kwa takribani wiki tatu chini ya Kocha Marcio Maximo kujiandaa na Ligi Kuu Bara iliyopangwa kuanza Septemba 20.

Kabla ya hapo, Yanga ilikuwa ikijifua jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuanza maandalizi hayo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic