August 18, 2014

CHEKA (KUSHOTO) AKIWA NA SALEH ALLY

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka ‘SMG’, amesema kamwe hawezi kufirikiria kupanda ulingoni kupigana na Mada Maugo akibeza kuwa uwezo wake ni mdogo.


Maugo hivi karibuni alifanikiwa kumchapa mpinzani wake, Thomas Mashali katika pambano la Usiku wa Matumaini na baada ya hapo akatamba kwamba anamtaka Cheka.

 Cheka amesema anamshangaa Maugo kuendelea kung’ang’ania kutaka kupigana naye licha ya kufahamu kuwa uwezo wake ni mdogo.

“Kiukweli namshangaa Maugo kuendelea kung’ang’ania kutaka kucheza na mimi, ila atambue kuwa uwezo wake ni mdogo, haniwezi, halafu ukiangalia rekodi zinaonyesha nilishampiga katika mapambano matatu.

“Unajua Maugo kwa kiwango chake anaweza kucheza labda na Kalama Nyilawila lakini siyo mimi au kama anataka nimuandalie pambano  yeye aje, kwa sababu sasa hivi nina kampuni yangu ya upromota na kesho (leo) kuna mabondia watacheza kwenye Ukumbi wa Vijana Social Hall hapa Morogoro,” alisema Cheka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic