August 18, 2014

GLOBAL FC


Timu ya Kampuni ya Global Publishers Limited, juzi Jumamosi ilipokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Dar City inayoundwa na wachezaji wengi wakubwa.
Katika mechi hiyo, Dar City iliongozwa na kipa wa Yanga, Hassani Hashimu aliyekuwa anaichezea Simba, Tippo Athumani, beki wa zamani wa Milambo na Coastal Union.
KAHABUKA

Wengine ni mshambuliaji wa zamani wa Simba, Clement Kahabuka, Baker Ranger na Chibwa walioonekana kuisumbua safu ya ulinzi ya Global Publishers iliyoongozwa na Jimmy Haroub na Khaleed Said.

Katika mchezo huo, Global ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 30 lililofungwa na Wilbert Molandi kwa kumchambua kipa wa Dar City.

Bao hilo halikudumu baada ya Dar City kusawazisha katika dakika 40 likifungwa na Kahabuka kabla ya kufunga mengine mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic