Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’, ameanza kujaribu kumtumia mshambuliaji wake wa kati, Amissi Tambwe kama kiungo wa pembeni huku akimpanga Elias Maguli nafasi ya kati.
Maguli amesajiliwa na Simba akitokea timu ya Ruvu Shooting ya Pwani
kwa ada ya uhamisho wa shilingi milioni 25.
Loga amesema amefanya uamuzi huo wa
kumhamisha namba Tambwe ili kuangalia uwezo wa Maguli ambaye alionekana kucheza
vizuri zaidi kwenye nafasi ya kati na kuna uwezekano mkubwa akaendelea nayo
msimu ujao wa ligi kuu.
“Nililazimika kumhamisha namba Tambwe ili nimuone huyu straika wangu
mpya, nimeona ni mzuri sana, akicheza namba tisa naamini nitaendelea kumtumia
kwenye nafasi hiyo katika michezo ya ligi kuu,” alisema Loga.
0 COMMENTS:
Post a Comment