LUIZIO |
Wakati Simba
ikiwa katika maandalizi yake
kuelekea Simba Day, siku ya Jumamosi ambapo itavaana na Zesco ya Zambia,
Mtanzania amewapa onyo.
Aliyekuwa
mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Juma Luizio, amefunguka kuwa Simba lazima
wajipange kutokana na timu hiyo kuwa vizuri kisoka, hivyo lolote linaweza
kutokea.
Simba inatarajia
kukutana na Zesco Agosti 9, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa katika mchezo wa
kirafiki ambapo timu hiyo itakuwa inaadhimisha siku yake maalum ya kuwatambulisha
wachezaji wake wapya.
Akizungumza kutoka nchini Zambia, straika huyo alisema timu yake hiyo mpya ipo
vizuri sana, hivyo Simba wanapokutana nao ni lazima waje kwa tahadhari kubwa.
“Zesco itavaana na Simba Jumamosi,
lakini napenda kusema wajipange tu kwa sababu timu hii ipo vizuri, wanatakiwa
kuja na tahadhari kubwa sana, kama unavyofahamu kwenye soka lolote linaweza
kutokea.
“Kwa sababu timu
hii ina wachezaji wengi wazuri kutoka nje, ndiyo maana inafanya vyema, japo
mpira siku zote hautabiriki, kikubwa tu wao wajipange na mimi naifahamu timu
hiyo pia,” alisema Luizio.
0 COMMENTS:
Post a Comment