JAJA |
Unaweza ukashangazwa na taarifa za washambuliaji wawili wa Yanga namna umaarufu wao
unavyozidi kupasua anga katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
COUTINHO |
Hata hivyo
inaonekana Yanga haitawapeleka Wabrazil hao kwenye michuano ya Kagame na badala
yake wataendelea kujifua hapa nchini.
Waandishi
mbalimbali wa vyombo vya habari wameiambia SALEHJEMBE kwamba Wabrazil
hao wanasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Rwanda na hasa wale
wa mji wa Kigali.
“Taarifa za
Coutinho na Jaja zinazidi kuwa gumzo, unajua watu hawaamini kama Yanga inaweza
kuwa imesajili Wabrazil, tena tumeelezwa makocha wawili pia ni Wabrazil,”
alisema Olvier Akaliza.
“Kwenye
vyombo vya habari wamekuwa wakizungumzia kuhusiana na hilo, utaona umaarufu wa
Yanga kwa hapa Kigali umepaa (umepanda) sana kutokana na Haruna (Niyonzima)
kuwa mchezaji wa Yanga.
“Hapa
Rwanda, Haruna anaheshimika sana. Hivyo wanapenda kujua timu yake inafanya vipi
na wengi sana wanaona kama ina Haruna na Wabrazil, basi itachukua kombe.”
Ukiachana na
Akaliza, mwandishi mwingine mkongwe nchini Rwanda, Clever Kazungu amesema wengi
wanapenda kuwaona Wabrazil hao wa yanga watafanya maajabu yapi.
“Unajua
Wabrazil kuja kucheza Afrika tena kwenye ukanda wetu, tayari imezua mjadala,
wengine wanasema watakuwa si wale wenye kiwango cha juu, wengine wanaona ndiyo
mapinduzi ya soka.
“Hivyo
wanasubiriwa hapa Kigali kwa hamu na kama kweli wakija, basi mechi za Yanga
zitakuwa zinajaza watu wengi sana,” alisema Kazungu.
Hata hivyo,
inaonekana Jaja na Coutinho watabaki Pemba kambini kwa kuwa kocha Marcio Maximo
ametenga vikosi viwili, kimoja kikiwa na vijana na wakongwe wachache kitakwenda
Kigali.
Wakongwe
ambao wanaonekana wataongozana na Leonaldo Leiva na Shadrack Nsajigwa watakuwa
ni Ali Mustapha, Omega Seme, Rajab Zahir, Hussein Javu, Nizar Khalfan na Said
Bahanuzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment