Washambuliaji
wawili wa TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wameungana na na
kikosi cha Taifa Stars mjini Maputo.
Kutua kwa
washambuliaji hao kumeongeza nguvu kwa Stars ambayo sasa iko kamili kwa mechi
ya kesho dhidi ya wenyeji Msumbiji.
Katika mechi
ya kwanza, Taifa Stars ililazimishwa sare ya mabao 2-2 katika mechi yakuwania
kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Hivyo katika
mechi ya kesho, kikubwa kwa Taifa Stars itakuwa ni ushindi tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment