August 6, 2014


ORIGI



Na Saleh Ally
WACHEZAJI 19 waliojiunga na vikosi vitano vya Ligi Kuu England, watakuwa na deni na sura zao tayari ziko kwenye kumbukumbu za mashabiki wa soka.


Usajili una maana kubwa kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakivutiwa nao, wakiamini wachezaji wapya wamekuwa ni changamoto ya kuboresha vikosi vyao.

Uongozi unaweza ukawa unaangalia suala la kuuza na kununua, kwamba umeingiza kiasi gani na faida ni nini. Pili ukaangalia suala la ushindi na mwisho kubeba kombe, lakini kwa mashabiki, jambo ni moja tu, ubingwa, full stop.
 
ALEXIS
Kwa England, hata kama soka lina miujiuza yake, lakini viko vitano vya Manchester City, Liverpool, Chelsea, Arsenal na Manchester United, ndiyo zenye uhakika kwamba moja wapo itakuwa bingwa msimu wa 2014-15.

Manchester City ndiyo mabingwa watetezi, Liverpool wanaulilia ubingwa zaidi ya miaka 20, Man United wamerejesha matumaini, Chelsea wana nyota ya makombe na Arsenal baada ya kubeba Kombe la FA, sasa wana imani wanaweza lolote.

Ushindani utakuwa mkubwa na wachezaji 19, waliojiunga na vikosi hivyo watakuwa na deni kwa kuwa wameingia sehemu ambazo zina ndoto ya mafanikio na kuchukuliwa kwao ni jawabu kwamba wasaidie kusukuma mabadiliko kwenye ubingwa.
 
CESC
Katika timu hizo tano, Manchester City ndiyo wenye mipango ya kutetea kombe hilo, lakini waliobaki kila mmoja anataka kulitwaa, hilo ni lengo namba moja. Lengo la pili ni kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
COSTA
Nafasi nne za juu ndiyo muhimu kwa kila timu ingawa ziko tano na nyingine kama vile Everton na Totthenham Hotspurs. Hivyo sura za wageni zinatupiwa macho kuwa zipi kati ya hizo mpya katika klabu hizo kongwe zitapeleka mafanikio.

 USAJILI:
ARSENAL
Walioingia
Alexis Sanchez (Barcelona-pauni 35m),
Mathieu Debuchy (Newcastle United-pauni 35m)
David Ospina (Nice-siri)
Calum Chambers (Southampton-siri)
Walioondoka
Lukasz Fabianski (Swansea City), Bacary Sagna (Man City-huru), Chuks Aneke (Zuite Waregem- huru), Nicklas Bendtner (huru), Chu Young Park (bure),Wellington Silva (UD Almeria-mkopo), Thomas Eisfeld (Fulham-siri) Carl Jenkinson (West Ham-mkopo).

 CHELSEA:
Walioingia
Cesc Fabregas (Barcelona-pauni 30m), Mario Pasalic (Hajduk Split-siri) Diego Costa (Atletico Madrid-pauni 32m), Filipe Luis (Atletico Madrid-pauni 20m), Didier Drogba (Galatasaray-huru).

Walioondoka
Tomas Kalas (Cologne-mkopo) Ashley Cole (Roma-huru),Samuel Eto'o (huru), Henrique Hilario (huru), Sam Hutchinson (huru), Frank Lampard (New York City-bure), Demba Ba (Besiktas-siri,  Mario Pasalic (Elche-mkopo). Lucas Piazon (Eintracht Frankfurt-mkopo), Patrick van Aanholt (Sunderland-siri) Romelu Lukaku (Everton-pauni 28m), Ryan Bertrand (Southampton-mkopo).

LIVERPOOL
Walioingia
Rickie Lambert (Southampton-pauni 4.5m), Adam Lallana (Southampton-pauni 25m), Emre Can (Bayer Leverkusen-siri), Lazar Markovic (Benfica-siri), Dejan Lovren (Southampton-siri), Divock Origi (Lille-pauni 10m).

Walioondoka
Luis Alberto (Malaga-mkopo), Michael Ngoo (huru), Stephen Sama (huru), Luis Suarez (Barcelona-siri), Iago Aspas (Sevilla-mkopo), Andre Wisdom (West Brom-mkopo).

MAN CITY:
Walioingia
Bacary Sagna (Arsenal-siri), Fernando (Porto-huru), Willy Caballero (Malaga-pauni 10m).

Walioondoka
Costel Pantilimon (Sunderland-huru), Joleon Lescott (West Brom-huru), Alex Nimely (Lille-huru), Marcos Lopes (Lille-mkopo), Gareth Barry (Everton-huru).

MAN UNITED:
Walioingia
Ander Herrera (Athletic Bilbao-pauni 28m), Luke Shaw (Southampton-pauni 32m).

Walioondoka
Federico Macheda (Cardiff City-huru), Jack Barmby (Leicester City-huru), Rio Ferdinand (QPR-huru), Ryan Giggs (kawa kocha), Nemanja Vidic (Inter Milan-huru), Alexander Buttner (Dynamo Moscow-siri), Patrice Evra (Juventus-siri).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic