August 2, 2014

MTIBWA SUGAR YA MSIMU ULIOPITA.


Uongozi wa Mtibwa Sugar umesema upo katika harakati za kutafuta wachezaji wawili ambao ni straika na kipa ili kukiongezea nguvu kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu.
Mtibwa imeweka kambi jijini Dar kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Matumaini dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Azam, unaotarajiwa kuchezwa Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar.
Ofisa habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru, alisema kwa sasa wapo sokoni kusaka wachezaji hao ambao wataziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya walioondoka kwenye kikosi hicho.
“Bado tupo katika kipindi cha usajili, tunazidi kujiimarisha kwa sababu timu yetu ni kubwa na ukiangalia wachezaji wetu wengi wameondoka, hivyo nafasi ambazo tunahitaji kuzijaza ni kipa na mshambuliaji mmoja,” alisema Kifaru.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic