August 2, 2014


MAXIME

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime, amesema kuwa hana muda wa kufuatilia viwango vya wachezaji walioomba kufanya majaribio na timu hiyo, badala yake akili yake ni kuangalia wachezaji wake tu.
Mtibwa ipo jijini Dar ambapo inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama, ikijiandaa na mchezo wa kirafiki wa Ngao ya Matumaini dhidi ya Azam hapo Agosti 8, mwaka huu.

Maxime amesema mpaka sasa kuna jumla ya wachezaji sita ambao wanatarajia kufanya majaribio wakiwemo Henry Joseph na Edward Christopher waliotokea Simba, lakini yeye amesisitiza kuwa hawezi kufuatilia maendeleo yao mazoezini kwake.

“Hapa hata ungekuwa na kipaji sasa hivi, ukiomba tunakukubalia, lakini akili yangu inawaangalia wachezaji wangu ambao nitakuwa nao keshokutwa katika michuano.

“Siwezi kuangalia maendeleo ya hao waliokuja kufanya majaribio, badala ya kuangalia wachezaji wangu,” alisema nahodha huyo wa zamani wa Taifa Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic