August 27, 2014

PHIRI AKIWA MAZOEZINI NA AMRI KIEMBA

Mohamed Selemani, Zanzibar
Kocha Patrick Phiri wa Simba, ametaka kikosi chake kuongezewa mechi ngumu.

Phiri raia wa Zambia amewaambia viongozi kuwa anataka ugumu wa timu wanazocheza nazo mechi za kirafiki uzidi kupanda ili kusaidia kukijenga kikosi hicho.
“Tunatafuta mechi ngumu zaidi kila baada ya mechi moja, haya ni maelekezo ya Kocha Phiri.
“Hivyo mechi zitazidi kuwa ngumu zaidi kuhakikisha tunajenga kikosi,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba kuhusiana na uamuzi wa kocha huyo.
Tayari Simba imecheza mechi moja na kuitwanga Kilimani kwa mabao 2-1.
Hata hivyo, Kilimani walionekana ni wepesi kuliko Simba na Phiri akasisititiza, taratibu kikosi chake kitakwenda kinafunguka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic