October 27, 2020


KIUNGO wa Simba, Bernard Morrison kuna hatihati akaukosa mchezo wa dabi ya Kariakoo unaotarajiwa kuchezwa Novemba 7 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga.

 Kwa mujibu wa Kanuni ya 39 (5)(5.2) mchezaji yeyote atayepigana au kupiga kabla ya mchezo au baada ya mchezo kumalizika basi atafungiwa michezo isiyopungua mitatu na faini isiyopungua sh. 500,00.


Pia Kanuni ya 39(6) mchezaji atayebainika kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu yanayojirudia au mara nyingi atafungiwa kucheza kati ya michezo 5 mpaka 10 na faini isiyopungua sh1m.


kutokana na kanuni hizo kama zitafuatwa kama zilivyo basi ni wazi kuwa mchezaji Morrison ataikosa Yanga kwa kuwa kanuni ya 35 inasema atafungiwa michezo 3 ambapo simba imebakisha michezo miwili ili kukutana na Yanga.


Kwenye mchezo wa Okotoba 26 uliochezwa Uwanja wa Uhuru kati ya Simba na Ruvu Shooting, Morrison alionekana akimpiga mchezaji wa Ruvu Shooting baada ya mchezo kusimama dakika ya 72 kutokana na kutokea kwa vurugu.


Vurugu hizo zilisababishwa na wachezaji wa Ruvu Shooting kugomea penalti waliyopewa Simba na ilipiga na John Bocco ambaye alikosa.


Kutokana na vurugu hizo mchezaji wa Ruvu Shooting, Shaaban Msala alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi wa kati ila BM hakuonyeshwa kwa kadi kwa kile ambacho ilionekana mwamuzi hajaona tukio hilo lililorushwa moja kwa moja na Azam Tv.

6 COMMENTS:

  1. Kweli we mchambuzi wa mchele na sio mpira. Yondani alipompiga mchezaji wa Mbao ulikuwa wa kwanza kukemea, leo hii kafanya Morisson kwa sbb ni mchezaji wa timu yako pendwa na wewe ndio engineer wa kila kitu umekaa kimya unaongea pumba tu! Shame on you!! Mungu si wa mmoja, wanafiki wote ipo siku mtaumbuka

    ReplyDelete
  2. Povu la nn wakati kila m2 aliona haina haja ya kumshambulia mtu hapa hebu tusubilihao Tanzania Football Failure watakuja na maigizo gani maana huu mpira wanakoupeleka siko kabisa. Ni full ubabaishaji tu, but iko siku inakuja huu ujinga wote utaisha kabisa.

    ReplyDelete
  3. Tusubirie Kamati yenye jina la masaa 72, itakuja na episode gan?

    Lkn hili la ngumi halivumiliki

    ReplyDelete
  4. Wasubiri amalize jambo lake na yanga ndo kamatibya masaa 77 ikae

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic