"Kwanza nitoe pole sana kwa matokeo mabaya mfululizo tuliyoyapata kwenye michezo yetu miwili mfululizo.
"Haya sio mazoea yetu,sio Simba tunayoitaka sisi,lakini ndio ukatili wa huu mchezo ulivyo na kiukweli hatuna budi kukubali yaliyotokea!
"Ndugu zangu najua inauma sana, lakini Simba ni klabu yetu na hatuna klabu nyingine tuipendayo toka moyoni zaidi ya hii.
"Inaweza kufikirisha kidogo Kama tunaweza kurudi katika nguvu yetu, lakini mimi Haji Manara nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba msimu huu hatutachukua ubingwa.
"Muhimu ni kujikosoa pale ambapo labda tunadhani tunateleza na kutorudia makosa ( Kama yapo) Ila mimi narejea kuwaambia inaweza kuwa upepo wa ukatili wa mchezo wenyewe wa mpira,ukizingatia katika mechi zote mbili tulipoteza nafasi kadhaa za kuweza kupata matokeo tofauti na tuliyoyapata!
"Kitu cha kufanya katika kipindi hiki kigumu kwetu ni kuwa na utulivu na kuwa wamoja, namaanisha UMOJA.
"Always (mara zote) Simba ikiwa MOJA huwa haishindwi hivi.
"Na kwa nini nasisitiza hili la UMOJA, hili tumeliandika katika mioyo yetu kama kauli mbiu yetu kuwa Simba Nguvu Moja, tukiliacha, hatujawahi kuwa Simba SC.
"Nimalizie kwa kuwaambia hiki ni kipindi mtacharurwa sana mitandaoni, maofisini na majumbani pamoja na vijiweni kwenu, ichukulieni hyo ndio raha na karaha ya football, isiwasambue hata kama itawaumiza. Naamini soon (karibuni) itageuka kwao, hatujalala ndugu zangu na hatutalala!
"Mimi mitandao yote naona kama imenielemea binafsi lakini nipo strong (imara) na bado imani yangu kuhusu Marathon hii ndefu ni kwamba tunakwenda kuchukua ubingwa wa nne mfululizo. Inshaallah."
Kwikwikwikwiiiiiiii, Manara ndio wakuyasema haya
ReplyDeleteMapenzi ya dhati ukisimamia unachokiamini ni ushindi tosha.
DeleteNdio mpira kila mtu kajipanga hakuna timu ndogo, ila tuwe tunazungumza ukweli utatusaidia, macho bado zipo nyingi sana waweza fungwa mechi mbili mwenzako akatoa sare macho 4 mnakuwa sawa bado
ReplyDeleteManara asiwe na kiherehere yeye ni msemaji wa timu asikimbilie kutoa matamko saa nyingine asubiri matamko rasmi ya timu
ReplyDeleteUkatili wa football unakuja pale team inacheza vizuri lakini inafungwa, kwa hizi match 2 timu haijacheza vizuri wala kutengeneza nafasi kama unavojaribu kutudanganya Manara sote tunaona wachezaji walivopoteza uwezo wa kujiamini, mpira haukai mguuni, shots on target zimekuwa nadra.. Kikubwa tumekuwa too dependant kwa kina Chama, Kagere, Fraga n.k. bila wao tunajikongoja tu, birian halionekani aisee
ReplyDeleteWachezaji wazawa WA simba hawapajui kupambana
ReplyDeletemikia fc,mipovu itawatoka sana mwaka huu,na bado vipigo vitaendelea tu
ReplyDeleteMikia fc wanakuwa wapi nguruwe nyie
ReplyDeleteTunaumia mashabiki nn tatizoo hasa
ReplyDeleteTatizo kubwa simba inamtegemea chama kutengeneza nafasi za magoli
ReplyDeleteTatizo kubwa simba inamtegemea chama kutengeneza nafasi za magoli
ReplyDelete