Anaandika Saleh Jembe
Bahati MBAYA, mchezo wa soka huwa hautoi furaha ya milele kwa UPANDE mmoja.
Tunaweza kujifunza msimu huu wa 2020/21 ikatusaidia kuongeza ufahamu kuhusiana na soka hata kama unaipenda vipi timu yako.
Ilikuwa vigumu kuamini Yanga ingeweza kuhimili mikikimiki hadi mechi angalau ya saba ikiwa imeshinda sita na sare moja kwa kuwa ilibadili nusu ya kikosi na ikaanza kwa kusuasua.
Azam FC walianza vema zaidi, wamepoteza kabla ya Yanga na Yanga wakishinda watakuwa juu yao. Simba yenye kikosi bora kwa kuchukua mara tatu mfululizo ubingwa, ndani ya mechi 7, wamedondosha pointi 8 huku wakipoteza pointi 6 katika mechi 2.
Hii inatoa funzo soka halitakupa kila unachotaka na hupaswi kuwa mwendawazimu au kuwehuka au kugombana na watu au kutukana hovyo kwa kuwa mchezo wa soka unapaswa ufurahiwe na wanaouelewa.
Angalia mwendo wa Yanga sasa, ni bora kabisa. Lakini hauwapi uhakika pia wa kila kitu, siku moja unaweza kubadilika na kuwa usiotarajiwa.
Soka mchezo wa kiungwana kwa maana ya kukubaliana na uhalisia na si uadui na chuki.
Tujifunze kukubaliana na nature ya mchezo wenyewe. Ukifungwa kubali, timu isipokuwa na performance nzuri tafakari, acha kukasirika na kulalama au kuwasingizia watu MANENO YA UONGO....
UKUMBUKE soka ni MGAWANYO WA FURAHA, leo UNASHINDA tu, kesho UTASHINDWA na yote yapokeee na kama unaona haiwezekani, basi CHAGUA MCHEZO MWINGINE WA KUUSHANGILIA.
Ila hata nyie waandishi mulipitiliza kuwasifia simba au mulikuwa kazini kuisifia kwa maslahi yenu ilikuwa timu ya kawaida ila kila kituo simba simba
ReplyDeletewell said
ReplyDeleteWaliwasifia Simba mpaka wakawatia Ujinga wachezaji,eti hata bila coach wanashinda, Sasa ndio matokeo yake.
ReplyDeleteKwakifupi msimu huu kiwago cha Simba kimeshuka
Si walisema wao wenyewe kwamba "watawakera sana?"..ndo kero hizo zimeanza.
DeleteMgema wa kibongo imsifie hadharani? wallah atatia ruvu yoote
Haha hii ndio soka inafuraisha unakasirisha ina kushangaza
ReplyDeleteKwa mara ya kwanza Saleh leo umeandika kitu cha maana sana kwetu sisi mashabiki wa hizi timu kubwa. Mchezo wa mpira ni katili kweli kweli. Yaani ni ngumu mno kukubali hiki kilicho ipata timu yangu pendwa Simba SC lakini ndio hivo tena; ni matokeo ya mpira hayo. Inabidi tujipange upya maana hakuna namna
ReplyDeleteHahahaaaaa naona wameamua kwel kuwakera mashabik wao tuliwambia hao wazee itafika wakat watakuwa wamechoka na ndo dalili zmeanza na baaaaaado
ReplyDelete