Yanga SC sasa rasmi imeondolewa kwenye michuano
ya Kagame kutokana na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati kupinga
kupeleka timu ya vijana.
Lakini Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye
akasema hizo ni dharau. Wanasema ni timu ina wachezaji wa timu ya kwanza, vipi Maximo abaki Dar es Salaam.
"Halafu timu isafiri kwenda kwenye mashindano makubwa kama ya Kagame. Huu ni utani, ndiyo maana sasa tumeipa nafasi Azam,"alisema jana.
Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC, watapambana
Kundi A lenye timu za Rayon Sport ya Rwanda, Coffee ya Ethiopia, Atlabara ya
Sudan Kusini na KMKM ya Zanzibar.
Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, KCC ya
Uganda, Flambeau de L’Est ya Burundi, Gor Mahia ya Kenya na Telecom ya Djibouti
wakati Kundi C linaongozwa na mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi, El
Merreikh ya Sudan, Polisi ya Rwanda na Benadir ya Somalia.
Rais Paul Kagame wa Rwanda ndiye mlezi wa
mashindano haya ambaye hutoa dola za Kimarekani 60,000 kila mwaka kwa ajili ya
zawadi.
Kwa kuwa Azam imechukua nafasi ya Yanga, sasa
itacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya wenyeji Rayon Sport Uwanja wa Amahoro
Agosti 8, mwaka huu.
Mechi ya saa 8 mchana itakuwa ni kati ya KMKM ya Zanzibar dhidi ya Atlabara ya Sudan
Kusini.
Mechi ya pili ya Azam FC itakuwa Agosti 10 dhidi ya KMKM, kabla ya kuivaa Atlabara Agosti 12, halafu itamaliza makundi dhidi ya Coffee ya Ethiopia Agosti 16.
yanga mnaniboa sana.....................hata kama mi ni shabiki namba moja, nimeboreka sana
ReplyDelete